UFUGAJI BORA WA NGURUWE
1.
Utangulizi
Nguruwe ni jamii ya wanyama wasiocheua, na wenye kwato zilizogawanyika.
Wanyama wengine walio kwenye jamii hii ni pamoja na Nguruwe pori na Ngiri
Nguruwe wanafugwa maeneo mengi duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita
Nguruwe ni kati ya mifugo iliyoonyesha ufanisi mkubwa wa kutoa nyama na fedha kwa
kipindi cha muda mfupi na hivyo kufanya kuwa aina ya mfugo anayapependwa kwenye
nchi mbalimbali kwa ajili hasa ya nyama na fedha
2.
Faida za ufugaji wa nguruwe
Nguruwe ni mnyama anayekuwa kwa haraka sana kuliko baadhi ya mifugo mingine
kama: Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo
Nguruwe huzaa na kuongezeka kwa wingi
Anauwezo wa kutumia mabaki yasiyowezekana kwa matumizi mengine
Anauwezo wa kutoa mafuta kwa ajili ya kupika
Anauwezo wa kutengeneza fedha za haraka kwa ajili ya uwezo wake wa kuzaa kwa
haraka na watoto wengi
Ni rahisi kuwalisha nguruwe
Wanaweza kukuzwa kwenye eneo dogo
Nyama yake ni laini na yenye viini lishe vingi
Huzalisha mbolea iliyobora kwa matumizi ya kilimo
3.
Aina za nguruwe
Humu nchini mwetu kuna kuu tatu za nguruwe
i. Nguzuwe wa kienyeji
ii. Nguruwe weye asili ya ugenini (Exotic breed)
iii. Nguruwe mchanganyiko (crosses): wenye mchanganyiko wa damu ya kienyeji na
ugenini ( Local x Exotic) na wenye mchanganyiko wa damu za ugenini (exotic x
exotic)
Aina za Nguruwe (breeds) wenye asili ya ujenini zinazopatikana kwa wingi kwenye
mazingira yetu.
i. Large white
Sifa
Rangi nyeupe
Miili mikubwa
Masikio yaliyosimama wima
Wana asili ya Uingereza
Wanauwezo wa kuzaa watoto wengi
Wana nyama nzuri
Wana uwezo mzuri wa ukuaji